31 Oktoba 2024 - 09:01
Habari Pichani | Mkutano mpya wa Waislamu Wafuasi wa Shule (Madrasat) ya Ahlul-Bayt (a.s) katika Mji wa "Chicago", Amerika

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul_Bayt (a.s) - ABNA - Zaidi ya Waislamu wapya 50 wanaofuata Shule (Madrasat) ya Ahlul-Bayt (a.s) na wakufunzi 10 kutoka maeneo yote Amerika, walikusanyika katika Mkutano ndani ya Jiji la " Chicago", Jiji lenye watu wengi zaidi katika jimbo la "Illinois". Mkutano huo ni wa muda wa siku tatu ili kuchunguza njia za kujenga Mustakabali wenye nguvu zaidi kwa jamii ya Kiislamu huko Amerika Kaskazini.